Romans 3:21-26

21 aLakini sasa, haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Torati na Manabii wanaishuhudia. 22 bHaki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa Isa Al-Masihi kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti, 23 ckwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, 24 dwanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Al-Masihi Isa. 25 eYeye ambaye Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwa sababu kwa ustahimili wake aliziachilia zile dhambi zilizotangulia kufanywa. 26Alifanya hivyo ili kuonyesha haki yake wakati huu, ili yeye awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yule anayemwamini Isa.

Umuhimu Wa Kuwa Na Imani

Copyright information for SwhKC